Habari za Mastaa

Trailer: Arnold Schwarzenegger yuko tayari kuileta ‘Terminator Dark Fate’ (+video)

on

Inaripotiwa kuwa Muigizaji wa filamu maarufu nchini Marekani Arnold Schwarzenegger yupo tayari kuileta filamu ya ‘Terminator Dark Fate’ ambapo inaelezwa kuwa  May 23,2019 iliachiwa trailer ya filamu hiyo.

Mpaka sasa trailer ya filamu hiyo imetazamwa na watu zaidi ya milioni 6 tokea iachiwe kwenye mtandao wa You Tube, pia huu ni ujio mpya baada ya miaka 28 iliyopita walipoitoa (Terminator 2: Judgement Day) mwaka 1991. Inaelezwa kuwa filamu hiyo imepangwa kuachiwa rasmi November,2019 ikiwa imeongozwa na James Cameron ambaye ameongoza filamu zote.

Gavana huyo wa jimbo la California tangu 2003 hadi Januari 2011 alijipatia umaarufu mkubwa duniani baada ya kufanya vizuri kwenye filamu nyingi ikiwemo Terminator 2 1991, True Lies 1994, The Terminator 1984, Commando 1985 na nyingine nyingi.

VIDEO: MAIMATHA KAZUNGUMZA WASHEREHESHAJI KULIPA KODI “MIMI NIMELIPA WAKALIPE WAEPUKE YA MC PILIPILI”

 

Soma na hizi

Tupia Comments