AyoTV

VIDEO: Fyeka Burundi Tusonge Qatar 2022 imezinduliwa leo

on

Waandishi wa habari za Michezo leo wamezindua kampeni ya uhamasishaji kwa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu World Cup 2022 nchini Qatar.

Kuelekea michezo hiyo ambapo Tanzania ataanzia Burundi Septemba 4 2019 na Septemba 8 kurudiana Dar es Salaam, kamati ya waandishi wa habari za michezo inayolenga kuhamasisha timu na watanzania kwa ujumla iliongea na vyombo vya habari, Mtangazaji wa Azam TV Fatuma Chikawe ni miongoni mwa waandishi walioongea.

“Leo tumezindua kampeni yetu mpya ya Fyeka Burundi Tusonge mbele, leo rasmi tunaitambulisha kwa watanzania wote kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia, tunaanza ugenini kisha tunarudi hapa nyumbani”>>> Fatma Chikawe

VIDEO: Niyonzima kaeleza kilichotokea kati yake na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments