Jukwaa la kutuma ujumbe la WhatsApp, lilianza tena huduma baada ya kukatika kote ulimwenguni kwa takriban dakika 20 siku ya Jumatano.
Mamia ya watumiaji duniani kote waliripoti kwenye mitandao ya kijamii kwamba hawakuweza kutuma ujumbe au kupiga simu kupitia programu kwa karibu saa moja.
Kampuni ya Meta inayomiliki WhatsApp, imekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa inarekebishwa.
Kampuni hiyo ambayo pia inamiliki Facebook na Instagram, haikueleza sababu ya kukatika kwa mtandao huo.
WhatsApp ina karibu watumiaji bilioni 2, na kuifanya kuwa chombo muhimu cha mawasiliano kwa biashara na serikali duniani kote.