Unaweza ukafanya kitu kwa mtu halafu akakupa tabasamu feki na ukahisi kwamba kafurahia kumbe ana lake moyoni.
Juzi siku ya Jumatatu Desemba 08, kulikuwa na taarifa kubwa kutoka Marekani inayohusiana na ziara ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William na Mke wake Kate Marekani ambapo walipata bahati ya kukutana na mastaa Jay Z, Beyonce pamoja na mchezaji wa Basketball kutoka timu ya Cavs, LeBron James.
Hiyo ilikuwa stori kubwa Marekani, hivi kumbe vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii Uingereza vilikuwa na story tofauti?
Picha aliyopiga staa wa Basketball, LeBron akiwa amemshika bega Kate kumbe amekiuka ‘protocol’ za falme ya Uingereza, huo ndio ulikuwa mjadala mkubwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari UK.
LeBron sio mtu wa kwanza kuvunja protocol hiyo, hata Michelle Obama aliwahi kufanya kosa kama hilo kwa kumkumbatia Queen Elizabeth II mwaka 2009.
Hapa kuna video inayoonyesha wakati LeBron akivunja ‘itifaki’ hiyo bila yeye mwenyewe kujua.
https://www.youtube.com/watch?v=G3B0aDUJNvg
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook