Michezo

Huu ndio uwanja wa Simba SC utakaoisaidia kuokoa Tsh 500,000/= kwa siku

on

Kwa zaidi ya miaka 80 toka imeanzishwa club ya Simba SC imekuwa ikikumbana na changamoto ya kumiliki miundombinu yake ya kufanyia mazoezi, kiasi cha club hiyo licha ya ukongwe wake kuishia kuishi maisha ya kukodi viwanja.

Simba SC kwa sasa inakaribia kuanza kutumia viwanja vyake vya mazoezi vilivyopo Bunju jijini Dar es Salaam, ili kuedana na matakwa ya viwanja vinavyotumika Ligi Kuu, Simba SC imejenga viwanja viwili Bunju cha nyasi bandia na nyasi za asili ili kufanya mazoezi kulingana na uwanja watakaocheza na mpinzani.

Kwa sasa inadaiwa kuwa club hiyo huwa inatumia kiasi cha Tsh 500,000/= kwa siku kwa ajili ya kulipia viwanja vya kufanyia mazoezi ya timu hiyo, kwa maana hiyo kama timu hiyo itafanya mazoezi kwa siku 20 katika mwezi, basi itakuwa imeingia gharama ya Tsh milioni 10 kwa ajili ya uwanja sawa na Tsh 100 ndani ya miezi 10.

VIDEO: BONDIA ARNEL TINAMPAY NAMBA 2 KWA UBORA PHILIPINE BAADA YA MANNY PACQUIAO KATUA DSM

Soma na hizi

Tupia Comments