Michezo

Ni mwaka wa Ronaldo? kingine alichomfunika Messi kiko hapa

on

Screen Shot 2014-05-30 at 3.25.04 AMCristiano Ronaldo ameendelea kumfunika mpinzani wake Lionel Messi baada ya kumshinda kwenye uchezaji bora wa dunia, ufungaji bora wa La Liga na Champions League, utajiri na sasa kwa mujibu wa taasisi ya uchunguzi na uchambuzi wa masoko ya Repucom, staa huyu wa Real Madrid ndio staa wa soka mwenye thamani kubwa kwenye masuala ya kibiashara.

Kwa mujibu wa Repucom, Cristiano ndio mwanasoka mwenye mvuto mkubwa wa kibiashara kwa makampuni makubwa duniani kutokana ufuasi mkubwa wa mashabiki alionao hata kupitia mitandao ya kijamii ambako ana likes zaidi ya millioni 82 kwenye Facebook, wakati anayemfatia ni Messi akiwa na likes millioni 57, kwenye twitter Ronaldo tena ameongoza kwa kuwa na wafuasi millioni 26.
ronaldo-vs-messi-portugal-argentina-national-team-captainsUtafiti huu pia umeonyesha Ronaldo anatambulika zaidi duniani kuliko wachezaji wenzie ambapo ameongoza kwa kupata asilimia 87% huku wachezaji wengine waliongia kwenye listi hiyo ya wachezaji wenye mvuto mkubwa wa kibiashara kulingana na umaarufu ni Cristiano Ronaldo, ni pamoja na Lionel Messi, Gerard Pique, Fernando Torres, Wayne Rooney  kwenye Top 5.

List kamili ipo hivi.

article-2641168-1E426A4D00000578-334_634x478-1Ili niwe nakutumia kila taarifa inayonifikia jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

Tupia Comments