Siku moja baada ya Rais wa club ya Simba Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za makosa matano likiwemo kosa la tuhuma ya utakatishaji fedha ambalo halina dhamana kisheria.
Hakimu Victoria Nongwa aliamua kuiarisha kesi hiyo hadi July 13 ndio itasikilizwa tena, huku Aveva na Kaburu wakirudishwa rumande, Simba leo wametoa taarifa kuwa kamati ya utendaji ya club hiyo itakutana kesho July 1 kwa ajili ya kikao ambacho kitaangalia shughuli za club zisikwame.
Kamati ya utendaji ya Simba itakaa kikao July 1 kuangalia namna ya shughuli za club zisikwame wakati huu Rais wao na makamu wakiwa rumande. pic.twitter.com/U0dSy8uvpJ
— millard ayo (@millardayo) June 30, 2017
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1