Top Stories

Huyu mfungwa aliekataa msamaha wa Rais Magufuli ana tatizo la akili (+video)

on

Jeshi la Magereza Mkoani Mbeya limetoa ufafanuzi kuhusiana na aliyekuwa mfungwa katika gereza la Ruanda Mkoani humo Meradi Abraham kugoma kutoka gerezani licha ya kuwa miongoni mwa wafungwa 259 walionufaika na msamaha wa Rais John Magufuli December 9 mwaka huu.

Meradi aligoma kutoka katika gereza hilo wakati taratibu za kuachiliwa huru zikiwa zimekamilika hadi alipotolewa na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakimtaka aungane na wenzake waliokuwa wakilakiwa na ndugu na jamaa zao baada ya kuwa raia wema.

HUYU ALIUA ATOKA GEREZANI KWA MSAMAHA WA MAGUFULI “NILIPIGANA DISCO, DAMU IKAVUJIA NDANI”

Soma na hizi

Tupia Comments