Ofisa wa Polisi, D/SSGT Arbogast ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mbunge wa Kawe Halima Mdee aliitisha mkutano na waandishi wa habari ili kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo.
Ofisa huyo wa Polisi ameyaeleza hayo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya kutupilia mbali kielelezo cha maelezo ya onyo kilichotolewa na upande wa mashtaka.
Hakimu Nongwa amesema ametupilia mbali kielelezo cha upande wa mashtaka kwa sababu maelezo ya onyo ya mshtakiwa yalichukuliwa nje ya muda.
Akitoa ushahidi wake Arbogast amedai kuwa yenye ndiye aliyemfanyia mahojiano Mdee ambaye alikiri kuitisha mkutano na waandishi wa habari, July 3, 2017.
Amedai kuwa mshtakiwa alimwambia ni kweli aliitisha mkutano na waandishi wa habari na lengo lake lilikuwa ni kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo.
Baada ya kutoa ushahidi huo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi, March 29, 2018 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
Naibu waziri alivyomfungia Roma leo na kumpa onyo Nay wa Mitego
“Watu hawana elimu kuhusu KUBEMENDA watoto” –Waziri Jafo