Marekani imeiondola vikwazo vya uchumi na biashara kwa nchi ya Sudan ikisema taifa hilo la Afrika lilikuwa limeanza kuangazia maswala kuhusu kukabiliana na ugaidi pamoja na ukiukaji wa haki za kibinaadamu dhidi ya raia wanaoishi katika jimbo la Darfur.
Uamuzi wa kuiondolea vikwazo Sudan pamoja na kusitisha vikwazo vya kiuchumi kwa taifa hilo umekuja mwezi mmoja baada ya Rais Donald Trump kuliondoa taifa hilo katika mataifa ambayo raia wake wamewekewa vikwazo vya kuingia nchini Marekani.
Hatahivyo uamuzi huo unaviacha vikwazo vingine kuendelea vikiwemo vile dhidi ya watu waliohusika katika uliofanyika katika eneo la Darfur.
Ulipitwa na hii? TCU imetaja idadi ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Vyuo Vikuu 2017/18