Top Stories

Baada ya kushikiliwa na Polisi Ester Bulaya apata dhamana akiwa Hospitali

on

Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya amepewa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na Wadhamini watatu pamoja na fedha Tsh. Milioni 20 na amepata rufaa ya kwenda kutibiwa Muhimbili.

Taarifa kutoka ripota wa Ayo TV na millardayo.com zinasema kuwa Mbunge huyo ameweza kudhaminiwa baada ya kushikiliwa na Polisi kwa siku mbili baada ya kumkata akiwa Hotelini huku pia akiruhusiwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Ester Bulaya aliwahishwa Hospitali jana usiku baada ya kuugua ghafla akiwa rumande na ameruhusiwa sasa kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupata matibabu ya awali katika Hospitali ya Wilaya Tarime.

Soma na hizi

Tupia Comments