‘MANENO YANAUMBA’ ni msemo ambao wengi huutumia na mmoja wa wanaouamini ni pamoja na Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe ambaye aliwahi kutabiriwa na wanafunzi wa kike wa Shule ya Msingi kuwa atakuwa Mbunge.
Kweli sasa yametimia ambapo kwa kukumbuka tukio hilo, Bashe leo August 19, 2017 kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe maalum kwa watoto hao akisema…>>>”Mwaka 2015 wakati namaliza mkutano ktk kiwanja cha Ushirika watoto hawa wakike Wakiwa wamevaa Uniform zao za shule ya Msingi Ushirika walinisimamisha wakasema maneno yafuatayo”
“Kaka Bashe sisi tunasali kanisani Kila Jpili sisi watatu kukuombea Ushinde na huyu Mwenzetu yeye huwa anakuombea kwenye madrasa Yao uwe Mbunge , nikawauliza kwanini mnaniombea Walijibu tu KITOTO tunakupenda”
“Mimi kwangu sikusahau hili jambo sikulichukulia kwa wepesi niliwatafuta Jana nimewapata Wako Form one na huyo Mdogo yupo darasa la Sita nimeenda kuwatembelea mtaani kwao na kuwaambia Maombi yenu Mungu aliyapokea nimeamua kuanzia sasa nitawasomesha na kuwagharamia Elimu yenu kadri Allah atakavonijaalia”
“Watoto hawa kwangu ilikua deni Hawakua wapiga kura bali walikua na Upendo na mimi na kitu peke ambacho waliweza kuona ni muhimu kunisaidia ni Maombi kwa Mungu ili niwatumikie that’s why my five yrs Agenda namba 1,2,3 ni Elimu AGenda namba 2 ni Afya .Upendo huo walonionyesha kwangu ni deni na mm Upendo nitakaowapa ni ELIMU Naomba Allah a nisaidie”
VIDEO: ALICHOKIONGEA HUSSEIN BASHE KUHUSU UJENZI WA RELI MPYA