Michezo

Shomari Kapombe tutamkosa AFCON 2019?

on

Beki wa Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Shomari Kapombe amekumbana na wakati mgumu katika maisha yake ya soka kufuatia kukumbana na jeraha linampa wakati mgumu kurejea uwanjani, Kapombe bado anapambana na jeraha hilo.

Matumaini ya Watanzania wengi ilikuwa ni kumuona Shomari Kapombe katika fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika Misri kuanzia June 21, Tanzania ikiwa imepangwa Kundi C na timu za Algeria, Senegal na Kenya, hivyo kujumuisha katika kikosi kwa Kapombe kulileta matumaini labda katika wachezaji 23 wa mwisho kwenda Misri atakuwepo.

Leo afisa habari wa timu Cliford Ndimbo amethibitsha kukosekana kwa mchezaji hiyo anayesumbuliwa na majeraha na imeoneka atakosekana katika AFCON “Kapombe amejitonesha akiendelea na mazoezi binafsi kabla ya kuungana na wenzake, kwa sasa hayuko na wenzake lakini anaendelea kufuatilia program ya mazoezi mpaka hapo mwalimu atakapotaja kikosi cha mwisho”

Kapombe amekuwa na wakati mgumu kupona majeraha hayo kutokana na kuumia, kama utakuwa unakumbuka vizuri Kapombe aliumia November 2018 akiwa nchini Afrika Kusini katika kambi ya maandalizi ya Taifa Stars katika mchezo wao dhidi ya Lesotho uliyochezwa Mjini Masseru, hivyo hadi sasa ni zaidi ya miezi 7 hajaonekana uwanjani.

VIA: Azam TV

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments