Michezo

Casillas ameruhusiwa kutoka hospitali lakini hajui hatma yake

on

Taarifa zilizoripotiwa May 1 2019 kutokea Ureno zilikuwa ni kuhusiana na golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na club ya Real Madrid Iker Casillas ambaye kwa sasa anaichezea FC Porto ya Ureno, kuwa alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuanguka ghafla akiwa mazoezini.

Casillas alianguka akiwa mazoezini na FC Porto kutokana na kupata mshituko wa moyo na kulazimika kukimbizwa hopitali kwa matibabu zaidi, tatizo ambalo lilipelekea kukaa hospitalini kwa siku kadhaa kabla ya leo May 6 2019 kuripotiwa ameruhusiwa kutoka hospitali ila hajui hatma yake kama atatakiwa kustaafu kucheza soka au kuendelea.

Kwa sasa Casillas ameruhusiwa hospitali na anaendelea vizuri na hali yake imeimarika na FC Porto wanapambana kuhakikisha staa huyo anaishi vizuri na afya yake izidi kuimarika zaidi, Casillas mwenye umri wa miaka 37 alijiunga na FC Porto 2015 baada ya kuichezea Real Madrid kwa miaka zaidi ya 15.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments