Baada ya kipigo cha magoli 3-0 cha UEFA Champions League cha FC Barcelona dhidi ya Liverpool katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliyochezwa Nou Camp, kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp ameeleza kuwa pamoja na kuwa ana mchezo mgumu wa marudiano lakini akili yake ipo dhidi ya Newcastle.
Klopp amekiri kuwa kufungwa dhidi ya FC Barcelona hakuwezi kuwaathiri wachezaji wake kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle, kwani kipigo kile hakiwezi kuwa haribu kisaikolojia wachezaji wake kwa namna yoyote ile kwani katika mpira ni kitu cha kawaida kufungwa kama unafikiria kushinda.
“Tunatakiwa tuthibitishe hilo katika mpira kama unataka kushinda inatakiwa ukubali pia kuwa bado unaweza ukapoteza vile vile, kiwango wachezaji walichokionesha unaweza ukahisi kabisa, tulicheza vizuri na kuwasababishia matatizo (Barcelona) lakini haikutosha usiku ule kwa sababu hatukumalizia(kufunga)”>>> Jurgen Klopp
May 4 2019 Liverpool watakuwa St James Park kucheza dhidi ya wenyeji wao Newcastle United, Liverpool wakicheza mchezo huo muhimu huku wakihitaji ushindi wakati wakimuombea mabaya Man City May 6 2019 apoteze mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Leicester City.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania