Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Patrick Aussems amethibitisha leo wataikosa huduma ya Erasto Nyoni

on

Club ya Simba SC inashuka katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza leo kuendeleza harakati zake za kutetea taji lake la Ligi Kuu Tanzania bara walilolitwaa msimu uliopita, Simba SC leo itacheza dhidi ya Alliance FC ambao ndio wenyeji wa mchezo huu.

Kocha Patrick Aussems amethibitisha Erasto Nyoni atakosekana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Alliance kutokana na kuugua. Wachezaji wengine ambao wataendelea kukosekana ni Pascal Wawa na Shomari Kapombe ambao wanasumbuliwa na majeruhi.

Simba SC inayokabiliwa na mfululizo wa mechi kutokana na kuwa na viporo vingi katika Ligi hiyo,. italazimika kutafuta ushindi katika kila mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania taji hilo licha ya kupoteza mchezo wake uliopita 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Simba kwa sasa wapo nafasi ya tatu wakiwa na point 60, Azam FC nafasi ya pili wakiwa na point 66 na Yanga wakiongoza kwa point 74 ila Yanga na Azam FC wamecheza michezo 32 wote wameizidi Simba michezo 8 ambayo hadi sasa imecheza michezo 24.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments