Michezo

Mc Gregor atangaza kustaafu MMA

on

Mchezo wa MMA (Mixed Martial Arst) leo unapoteza moja kati ya washindani wenye majina makubwa katika mchezo huo Conor McGregor ambaye ameamua kutangaza rasmi kustaafu na kuendelea na maisha mengine baada ya kucheza kwa muda mrefu.

Nyota wa mchezo wa MMA (Mixed Martial Arts) Conor McGregor mwenye umri wa miaka 30 ametangaza kustaafu kucheza mchezo huo kupitia akaunti yake ya Twitter, McGregor hajapigana toka October mwaka jana alipopoteza pambano dhidi ya Khabib Nurmagomedov.

McGregor hadi anatangaza kustaafu mchezo huo alikuwa amecheza mapambano 25 akipoteza mapambano manne  na kushinda mapambano 21, Mc Gregor aliwahi pia kupigana katika mchezo wa Boxing na bondia Floyd Mayweather na kupoteza.

MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS

Soma na hizi

Tupia Comments