Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

Kocha wa Kenya kakiri “Huwezi kulinganisha Taifa Stars akicheza Samatta, Msuva na Ulimwengu”

on

Kocha Mkuu wa Harambee Stars Sebastian Magne amefunguka kuhusiana na mchezo wake dhidi ya Taifa Stars uliomalizika kwa sare tasa 0-0, Magne amesema kuwa utofauti ni mkubwa kutokana na kucheza na kikosi kipya ambacho hakina wachezaji aliocheza nao AFCON na kama ametoa nafasi kwa vijana hivyo hata yeye anaamini hii sio Taifa Stars ngumu kama angekuwepo Msuva, Samatta na Ulimwengu.

“Kwetu ilikuwa ni ngumu kabla ya mchezo sababu wachezaji wangu karibia 15 wamekosekana kwa hiyo tunatengeneza timu mpya kwa siku chache ni ngumu baada ya AFCON hatukuwa na muda mwingi, tofauti ni kuwa ya wachezaji waliocheza AFCON na hawa huwezi kulinganisha ukicheza na Tanzania ikiwa na Samatta, Msuva na Ulimwengu”>>>Sebastian Megne

Baada ya mchezo wa leo wa Tanzania kuwania kucheza CHAN 2020 kumalizika kwa sare tasa 0-0, sasa Taifa Stars itakuwa na safari ya kwenda Kenya kucheza mchezo wa marudiano August 4 huku wakihitajika kupata sare ya 1-1 au ushindi ili kusonga hatua inayofuata.

VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6

Soma na hizi

Tupia Comments