Michezo

Baba mzazi wa Neymar kaua uvumi wa mwanae kwenda Real Madrid

on

Wakati kukiwa na tetesi kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar kuwa anaweza kuihama club hiyo, kwa madai ya kupata presha kubwa kutoka kwa wakongwe wa Brazil kuwa kama anataka kuwa mchezaji bora duniani na kushinda tuzo anapaswa kuwa katika club na Ligi ya Juu.

Baba mzazi wa mchezaji huyo Neymar Senior ameweka wazi kuwa mwanae anaweza kuendelea kuitumikia Paris Saint Germain kwa miaka mingine tena, kauli hiyo imekuja baada ya baba wa Neymar kuweka wazi kupitia UOL Sporte kuwa “Tayari tumeshafanya mazungumzo na PSG ya kuongeza mkataba”

Taarifa hizo zinakuja kukiwa na tetesi kuwa mtoto wake yuko mbioni kujiunga na Real Madrid ya Hispania mwishoni mwa msimu hivyo ameua uvumi huo, kama utakuwa unakumbuka vizuri wachezaji na wakongwe wa Brazil kama Rivaldo aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa kama Neymar anataka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia arudi Hispania ila kwa Ligi ya Ufaransa haoni uwezekano huo.

MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS

Soma na hizi

Tupia Comments