Kuelekea michezo ya robo fainali ya michuano ya CAF Confederation Cup shirikisho la soka Afrika CAF limetangaza kumfungia mchezo mmoja kukaa kwenye benchi kocha mkuu wa club ya Gor Mahia ya Kenya Hassan Oktay kutokana na kumlalamikia muamuzi wa mchezo.
Hassan Oktay amekutana na adhabu hiyo baada ya kubishana na refa wa mchezo wa mwisho wa Kundi D wa Gor Mahia dhidi ya Petro Atletico ya Angola, kiasi cha kufikia kutolewa katika benchi dakika ya 54 mchezo huo ambao Gor Mahia walipata ushindi wa goli 1-0.
Hivyo Gor Mahia watamkosa kocha wao Hassan Oktay katika game yao ya kwanza ya robo fainali April 7 2019 wakiwa nyumbani katika uwanja wa Moi dhidi ya RS Berkane ya Morocco, pamoja na hayo watawakosa wachezaji wao Harun Shakava, Shaffik Batambuze, Jacques Tuyisenge na Ernest Wendo kwa kutumikia adhabu, huku Tuyisenge na Batambuze wao watawakosa michezo yote miwili.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars