Michezo

Pogba kajibu tuhuma za Roy Keane “Siwezi kuamini  aliyoyasema”

on

Kabla ya kuchezwa game ya Manchester Derby kati ya Man United dhidi ya Man City, kiungo wa zamani wa Man United Roy Keane alinukuliwa na vyombo vya habari kwa kumtuhumu Paul Pogba hadharani kuwa ana husika na baadhi ya makosa mengi yanayopelekea Man United kukosa ushindi.

Kauli ya Keane kumlaumu Paul Pogba ilianza baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wao wa ugenini wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton kwa kufungwa 4-0, Keane alifika mbali zaidi kuhusiana na kiwango cha Pogba katika mchezo ule kiasi cha kusema yeye (Keane) sio shabiki wa Paul Pogba.

Baada ya kusikia kauli za Keane, staa huyo wa Ufaransa alijibu kwa kusema “Siwezi kuamini  maneno aliyoyasema, hakuna tatuzo anaweza kusema anachokitaka analipwa kwa kazi hiyo, silipwi kwa ajili ya kuongea nalipwa kwa kazi yangu uwanjani na kuipambania timu”

Man United kwa sasa ina hati hati ya kukosa nafasi ya kushiriki UEFA Champions League msimu wa 2019/2020, hiyo inatokana na kuwa na wakati mgumu wa kumaliza TOP 4 katika msimamo wa Ligi Kuu England, Man United kwa sasa ipo nafasi ya 6 katika EPL na imesalia na game mbili Ligi kumalizika wakiwa na point 65, kumaliza kwao TOP 4 kuna tegemeana na ushindi katika michezo yote miwili huku akiwaombea Chelsea na Arsenal wapoteze game zao.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments