AyoTV

Amunike kaita 39 Taifa Stars, kataja kigezo kitakachotumika kupata 23 AFCON 2019

on

Mapema leo asubuhi kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Emmanuel Amunike alitaka kikosi cha wachezaji 39 wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars watakaoshiriki kucheza michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019, Amunike ametaja majina ya wachezaji 39 wa kikosi cha awali.

Amunike ametaja kikosi hicho lakini ana mtihani wa kuhakikisha anafanya maamuzi sahihi kwa kuchuja majina 23 ya kikosi cha mwisho kitakachoshiriki AFCON 2019 nchini Misri, hivyo kati ya 39 atatakiwa kukata majina ya wachezaji 16 na kubakia 23.

Emmanuel Amunike ameeleza kuwa sababu ya kuwaita wachezaji wengi hivyo ni kutokana na kuwa chochote kinaweza kutokea kuna kupata majeraha, lakini kuangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kabla ya kufanya maamuzi, kigezo chake kikuu atakachokitumia ni kiwango cha mchezaji mmoja mmoja.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments