Michezo

JS Saoura wamewadhihirishia Al Ahly kuwa Kundi D gumu

on

Simba SC wanasubiria leo kucheza game yao ya pili ya Kundi D hatua ya Makundi ya CAF Champions League,wenzao Al Ahly ya Misri na JS Saoura ya Algeria nao walicheza game yao ya pili nchini Algeria, hiyo ni baada ya Al Ahly mchezo wa kwanza kuanzia nyumbani na JS Saoura kuanzia ugenini dhidi ya Simba, JS Saoura ni timu inayochezewa na mtanzania Thoma Ulimwengu na leo alicheza dhidi ya Al Ahly akitokea benchi.

Game ya JS Saoura dhidi ya Al Ahly ilitarajiwa kuwa Al Ahly angeweza kuchukua point tatu kirahisi kutokana na timu hiyo kuhisiwa kama timu nyepesi kufuatia kipigo cha magoli 3-0 waliyofungwa na Simba katika game ya kwanza, Ah Ahly wamekutana na JS Saoura ya tofauti ambayo nusura wapoteze mchezo baada ya JS Saoura kufunga goli la kuongoza kupitia kwa Cherif na kudumu hadi dakika ya 85 Al Ahly waliposawazisha kupitia kwa Nedved.

Hata hivyo dakika za lala salama JS Saoura walipata goli ila lilikataliwa na muamuzi, kwa maana hiyo matokeo hayo yanaifanya Al Ahly iongoze Kundi D kwa kuwa na point 4, wakifuatiwa na Simba SC walio na point tatu, JS Saoura nafasi ya tatu wakiwa na point moja na AS Vita wakishika mkia kwa kuwa hawana point ila Simba na AS Vita wote wamezidiwa mchezo mmoja.

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments