Top Stories

Hii ni kutoka chama cha wahasibu Tanzania (TAA)

on

Chama cha wahasibu Tanzania (TAA) vimekutana na viongozi wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania, Jukwaa la Wafanyabiashara (JWT), bodi ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) katika kongamano la pamoja lililowakutanisha Muhasibu House kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na taaluma hiyo.

Kongamano hilo lililofanyika na kwakuwakutanisha Marais wa vyuo vikuu mbalimbali Tanzania, mwenyekiti wa TAA Dr Fred Msemwa ameeleza kuwa lilikusudia kuwajenga kimawazo na ishu za ajira sambamba na kuwasajili wanafunzi wote wanaosoma masuala ya uhasibu katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Pamoja na kuwa TAA imeanzishwa toka 1983 inakumbana na changamoto kutoka kwa wasomi wa taaluma hiyo kutojisajili kwa wingi katika chama hicho, ukizingatia ndani ya miaka 36 toka kuanzishwa kwake ina jumla ya wanachama 1500 pekee kati ya hao 1250 ni wahasibu  na wakaguzi, huku 250 wakiwa ni wanafunzi waliojiunga na chama hicho wakiwa bado wanasomea taaluma hiyo.

Noel Lewis wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) “Tumeshapaza sauti zetu katika majukwaa mbalimbalimbali, ikiwemo Bungeni, hivyo tunaamini serikali itasaidia kutatua changamoto zetu wafanyabiashara hasa katika masuala ya kodi”

Dhumuni kubwa la kongamano hilo lililenga kuhamasisha wasomi wa taaluma ya masuala ya fedha na uhasibu kujiunga na kuongeza nguvu kwenye chama hicho, sambamba na kujenga muamko kwa wanafunzi wa taaluma hiyo kuona umuhimu wa kujiunga na TAA, baadhi ya marais wa vyuo hivyo waliohudhuria wa vyuo vya Dodoma, Dar es Salaam, Mzumbe, Ushirika Moshi, St John Dodoma, IAA Arusha, TIA, Chuo Kikuu Iringa na IFM.

Mtanzania anayefanya biashara ya jongoo, tandu, chura na konokono kwa miaka 22

Soma na hizi

Tupia Comments