Habari za Mastaa

Jay Z ashtakiwa kwa kumsabishia Mwanamasumbwi matatizo kichwani

on

Inaelezwa kuwa Rapper Jay Z ameshtakiwa na Mwanamasumbwi Daniel Franco’25 kwa kutojali baada ya kumlazimisha kupigana akiwa hajaridhia kitendo hicho na baadae kudai kuwa alipata matatizo kwenye ubongo wake. 

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Blast’ umeripoti kuwa Daniel Franco alisaini dili na kampuni ya michezo ya ‘Roc Nation Sports’ mwaka 2015 na aliwahi kutajwa kwa kuweka rekodi ya 10-0-3 akiwa na ushindi wa mara saba kupita TKO. Daniel alisema kuwa alishinda mashindamo matano ya mwanzo akiwa chini ya Roc Nation.

Daniel Franco pamoja na baba yake walitoa taarifa kwa Roc Nation na kusema kuwa Franco hakuweza kupigana March 23, 2017 kwa sababu alikua mgonjwa na baadae ilidaiwa kuwa kampuni hiyo ilimuamuru apigane. Franco alikosa ushindi kwenye pigano lake la nane kutokana na kupata matatizo kwenye ubongo wake na kupelekea kufanyiwa upasuaji.

Inaelezwa kuwa mwaka 2017 familia ya Daniel iliomba msaada wa pesa za matibabu kutoka kwa Roc Nation lakini hawakupatiwa hivyo Franco anaishtaki kampuni ya Roc Nation , Live Nation na Jay Z binafsi kwa kutomjali. 

VIDEO: “MUNGU ATUPE NINI KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA TANO IMETOKA BILLION 4, KUCHUKUA MKOPO BILA RIBA”

Soma na hizi

Tupia Comments