Michezo

Simba SC haondoki mtu!! Aishi Manula hadi 2022

on

Club ya Simba SC licha ya kutangaza kuwa watafanya maboresho makubwa katika kikosi chao lakini inaendelea kujihakikishia kuwa wachezaji wake muhimu hawaondoki katika timu yao, kuelekea maandalizi yao ya mwakani Simba SC imetangaza kumuongezea mkataba kipa wake Aishi Manula.

Simba SC leo imemtangaza rasmi Aishi Salum Manula kuwa wamemuongezea mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia Simba SC, hiyo ikiwa ni siku moja imepita toka Simba SC itangaze kumuongezea mkataba John Bocco.

Kwa sasa Aishi Manula yupo kambini Cairo Misri akijiandaa na Taifa Stars kwa ajili ya fainali za AFCON 2019, Manula alijiunga na Simba SC kama mchezaji huru miaka miwili iliyopita akitokea Azam FC ambayo walishindwa kufikia makubaliano.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments