Michezo

Liverpool imetoa zawadi ya Iphone za dhahabu kwa wachezaji wake

on

Baada ya miaka 14 club ya Liverpool bila kuwa na taji la UEFA Champions League, hatimae June 1 2019 walifanikiwa kutwaa taji hilo kufuatia kuwafunga Tottenham kwa magoli 2-0, taji hilo limewafuta machozi na kuwatulizi majonzi ya kuendeleza kuliwania taji la EPL kwa mwaka wa 30 bila mafanikio.

Kufuatia Ubingwa huo ambao kwao wa sita wa UEFA Champions League kihistoria, wachezaji wa Liverpool pamoja na kuwa na utajiri wa fedha lakini wamezawadia zawadi ya Iphone X toleo maalum kwa ajili ya wachezaji wote waliofanikisha kutwaa Ubingwa huo.

Liverpool wamepewa zawadi ya Iphone X zilizonakshiwa na dhahabu, hilo likiwa ni toleo maalum kwa ajili yao, Iphone hizo zinathamani ya pound 3500 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 10 na kila Iphone ina jina la mchezaji wa Liverpool na namba ya jezi yake.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments