Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

VIDEO: Haji Manara kafunguka, vipi kaondolewa Simba SC?

on

Baada ya kuwepo kwa zaidi ya wiki moja ya tetesi kuwa afisa habari wa sasa wa Simba SC Haji Manara anaondolewa katika nafasi hiyo na kurithiwa na Gift Macha wa Azam TV, leo Haji Manara kafunguka kuhusiana na hilo.

Simba SC hivi karibuni walitangaza nafasi za kazi na watu mbalimbali waliomba nafasi hizo ikiwemo ya Media Officer wa Simba SC, indaiwa kuwa watu wote waliomba nafasi hizo ila Haji Manara hakuwa ameomba, hiyo ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya club ya Simba SC kwenda katika mfumo wa hisa.

Sasa katika mkutano wa waandishi wa hanari Haji Manara leo ameongea na waandishi wa habari, vipi kuhusiana na nafasi yake Simba SC anaondoka, vipi kuhusiana na anachoandikwa yuko mbioni kuachia ngazi Simba SC.

“Nafasi zipo nyingi za Simba SC kwani ni Haji Haji Haji mbona nafasi zipo nyingi zimetangazwa lakini kwa nini Haji? ngoja niwaambie ndugu zangu, hiki kiti cha usemaji wa Simba ambacho nimekikalia hapa sitakaa nacho milele na hakuna mtu yoyote atakayekaa nacho milele”>>>Haji Manara

adada

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments