Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta anendelea kuwa mwiba mkali kwa timu pinzania kwa kuendelea kuonesha ubora wake katika kila mchezo anaocheza kwa kufunga na wakati mwingine kutoa assist.
Samatta akiwa sehemu ya kikosi cha KRC Genk kilichokuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Luminus kucheza game yake ya 7 ya Play Off ya Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Antwerp FC katika uwanja waop wa Luminus, walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-0, Samatta akipachika goli la pili dakika ya 55.
Goli la kwanza la KRC Genk lilifungwa na Malinovsky kwa penati dakika ya 35 la tatu, Ito dakika ya 57 na mwisho likafungwa tena kwa penati na Heynen dakika ya 90, ushindi huo umeifanya KRC Genk iendelee kuongoza katika msimamo wa game za Play Offs kwa kuwa na jumla ya point 50 wakicheza game 7 na wamesalia na game tatu huku wakifuatiwa na Club Brugge walioko nafasi ya 2 kwa kuwa na point 41 wakicheza game 6 na wamesalia na game 4.
Mbwana Samatta anayeongoza kwa wafungaji magoli katika Ligi hiyo ya nchini Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro League kwa kufunga jumla magoli 23, wakiwa wamesalia mechi tatu sawa na kupambania point 9, ili wawe Mabingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu watatakiwa kuvuna point 4 kati ya 9 zilozobaki ili kuwa Mabingwa, hivyo Genk na Samatta wanasubiri muda tu uamue.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania