Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni ameendelea na mpango wake wa kuhakikisha anatokomeza biashara ya uuzaji wa dawa za kulevya visiwani Zanzibar, hayo ameongea baada ya kuwasili visiwani humo na kukutana na viongozi wa Polisi wanaohusikana na usimamizi wa hilo.
Katika mkutano wake na wazi mbele ya waandishi wa habari ameeleza ni fedhea kubwa kwa kisiwa kama cha Zanzibar chenye idadi ya watu milioni 1.3, kushindwa kudhibiti janga la uuzwaji wa dawa za kulevya, Masauni amekiri kuwa hawezi kuvumilia uzembe wa watu wachache katika hilo.
Waburundi 11 wamekamatwa wakilima Bangi Kigoma (+video)