AyoTV

Nahodha wa Uganda akiri haitakuwa rahisi kuifunga Serengeti Boys kesho

on

Baada ya kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys kuongea na waandishi wa habari, ilifika zamu ya wapinzani wao Uganda The Cranes U-17 kuongea na waandishi wa habari na kuelezea mipango yao kuelekea mchezo huo.

Mchezo wa kesho ni muhimu kwa timu zote Uganda na Tanzania kutokana na timu hizo kupoteza michezo yao ya awali, hivyo yoyote kati ya Uganda na Tanzania atakayepoteza mchezo huo atakuwa ameyaaga rasmi mashindano hayo na kukatisha rasmi matumaini ya kukata tiketi ya kwenda Brazil katika fainali za Kombe la Dunia la vijana U-17.

Kuelekea mchezo huo nahodha wa Uganda The Cranes U17 Kizito ameongea na waandishi wa habari “Tulipoteza mchezo wetu wa kwanza haina maana kuwa ndio tumetolewa katika mashindano, tuna mchezo pia wakucheza na Tanzania, hii ni mara ya pili tunacheza na Tanzania mara ya mwisho tulicheza nao katika nusu fainali ya (Cecafa)lakini haina maana kuwa tutashinda”>>>Kizito 

Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?

Soma na hizi

Tupia Comments