Baada ya club ya Juventus kutangaza kuwa haitoendelea tena na aliyekuwa kocha wao Massimiliano Allegri katika msimu wa 2019/2020, wengi wameanza kuhusisha majina ya makocha mbalimbali kama ndio watakwenda kuwa mbadala wa kocha huyo aliyedumu katika club hiyo kwa miaka mitano.
Juventus imeamua kuachana na kocha Massimiliano Allegri kutokana na kutofurahishwa na hatua wanayoishia katika michuano ya UEFA Champions League, kwani wanataka kocha anayeweza kuwaletea taji hilo, kwa misimu yote mitano kocha Massimiliano Allegri aliyekuwepo Juventus amefanikiwa kutetea taji la Ligi Kuu ya Italia Serie A kwa mara zote.
Kuelekea maandalizi ya msimu ujao Juventus wameanza kuhusishwa kuwa mbioni kuingia mkataba na makocha mbalimbali wakiwemo Antoine Conte, Simone Inzaghi, Diego Simeone, Maurizio Sarri, Carlo Ancelotti, Mauricio Pochettino, Jose Mourinho na Pep Guardiola ambao ndio wanatajwa ila Pep Guardiola amekanusha kuwa haendi Juventus.
“Mara ngapi nimekuwa nikisema siendi Juventus au Turin? Sitahamia Italia nitabakia hapa (Man City) kama watanihitaji kwa misimu miwili na zaidi nina mkataba siwezi kuhama, nimeridhishwa na hii club na hawa watu hapa siendi popote”>>>Pep Guardiola
Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC