Habari za Mastaa

Chris Brown ataja tarehe atakayoachia Album yake mpya, afanya ngoma na Drake

on

Mwimbaji wa RnB Chris Brown ameweka wazi tarehe ya ujio wa Album yake ya tisa ‘Indigo’ na kusema kuwa itaachiwa rasmi June 21,2019 ikiwa na jumla ya ngoma 30 mkali huyo aliyasema hayo kupitia sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika May 5,2019.

Album hiyo inatajwa kujumuisha ngoma ambazo tayari zimeshaachiwa ikiwemo “Undecided,” “Back to Love”,  wageni waalikwa siku ya uzinduzi wa Album hiyo wanatajwa kuwepo mastaa kama Justin Bieber, Tory Lanez, Tyga, H.E.R., Joyner Lucas, Gunna Nicki Minaj, G-Eazy na Juicy J na unaambiwa kuwa tayari Chris Brown kashafanya kolabo na rapper Drake kama ilivyoahidiwa miezi kadhaa iliyopita.

Chris Brown aliweka rekodi ya kufikisha wiki 400 ndani ya chart za album (Billboard 200) baada ya album yake iliyopita ‘Heartbreak On A Fool Moon’ kufikisha wiki ya 77 mpaka sasa tangu itoke October 31, 2017 ikiwa na jumla ya ngoma 45.

VIDEO: MKE WA ASKOFU GWAJIMA ‘MIMI NI JASIRI KAMA SIMBA, MUME WANGU NAMFAHAMU’

Soma na hizi

Tupia Comments