Michezo

Yaya Toure ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka

on

Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast aliyewahi kuvichezea vilabu vya Man City ya England na FC  Barcelona Yaya Toure ametangaza kustaafu kucheza soka leo akiwa na umri wa miaka 35, Toure ambaye aliondoka Man City kwa madai ya ubaguzi wa kocha wa timu hiyo Pep Guardiola ameamua kuachana na soka na kuendelea na maisha mengine.

Toure amefikia maamuzi hayo licha ya awali aliripotiwa kuwa na mpango wa kurudi England kuendelea kucheza soka, Toure hadi anastaafu soka alikuwa amewahi kuvichezea vilabu vya Beveren ya Ubelgiji (2001-2003), Metalurh Donetsk ya Ukraine (2003-2005), Olympiacos ya Ugiriki (2005-2006), Monaco ya Ufaransa (2006-2007), FC Barcelona ya Hispania (2007-2010), Man City ya England (2010-2018) na Olympiacos ya Ugiriki 2018.

Pamoja na kucheza jumla ya 6, Yaya Toure hadi anatangaza kustaafu kucheza soka alikuwa amecheza jumla ya mechi za ushindani 600, game 101 zikiwa za timu ya taifa na kufunga jumla ya magoli 119, Toure ametwaa jumla ya mataji 15, EPL mara 3, LaLiga 2, League Cup 2, Champions League 1, Copa Del Rey 1, Supercopa de Espana 1, Super Cup 1, Club World Cup 1, FA Cup 1, Ngao ya Hisani 1 na AFCON 1.

Samatta kaweka historia Ubelgiji, mchezaji wa tatu kuwahi kushinda Ebony Award 2019

Soma na hizi

Tupia Comments