Michezo

Diego Godin muda wake Atletico Madrid umeisha

on

Baada ya kudumu na club ya Atletico Madrid ya Hispania kwa miaka 9 beki wa kati wa kimataifa wa Uruguay Diego Godin, ametangaza rasmi kuwa ataondoka katika club ya Atletico Madrid mwisho wa msimu wa 2018/2019.

Godin mwenye umri wa miaka 33 anaondoka Atletico Madrid aliyojiunga nayo 2010 akitokea Villarreal pia ya nchini humo, kuondoka kwa Diego Godin ambaye ni nahodha wa timu hiyo kunatajwa kuwa anahama Ligi hiyo kabisa.

Hivyo tetesi za kuwa atajiunga na Inter Milan ya Italia zinapata nguvu zaidi, Diego Godin ambaye alitangaza taarifa hizo huku akimwaga machozi, toka amejiunga na timu hiyo akitokea Villarreal ameichezea jumla ya michezo 387 na kuifungia magoli 27 ambapo alisaidia club hiyo kutwaa taji lao la kwanza la LaLiga.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments