AyoTV

VIDEO: Kocha wa Kagera Sugar kakikiri “Simba ni moja kati ya timu 4 Afrika”

on

Timu ya Simba baada ya kupata kipigo mara tatu mfululizo kutoka Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba, leo wamefanikiwa kuibuka na Ushindi wa mabao 3-0, magoli ya Simba SC yakifungwa na Meddie Kagere aliyefunga mawili dakika ya 4 na 78 kwa mkwaju wa penati.

Goli la pili likafungwa na nahodha wao msaidizi Mohamed Hussein Tshabalala dakika ya 36 ya mchezo, mchezo huo umewafanya Simba kufikisha jumla ya point 9 sawa na Kagera Sugar walio na point hizo ila wameizidi Simba SC mchezo mmoja.

Baada ya mechi hiyo makocha wa zote mbili kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime ameeleza kuwa Simba kwa sasa ni miongoni mwa timu kubwa nne Afrika ndio maana wamewafunga, wakati kochja wa Simba SC Patrick Aussems ameongea kuwa yeye sio kocha wa kuongea bla bla kama wengine anatafuta matokeo tu.

VIDEO: Antonio Nugaz kaanza na Mbwembwe Yanga “Yanga unyonge kwisha”

Soma na hizi

Tupia Comments