Michezo

Taifa Stars yafuzu kucheza fainali za CHAN 2020 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo ilikuwa nchini Sudan katika jiji la Khartoum kucheza mchezo wao wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza fainali za CHAN 2020 dhidi ya Sudan, Tanzania ilienda Sudan ikiwa imepoteza 1-0 katika mchezo wake wa kwanza jijini Dar es Salaam.

Tanzania ikiwa Sudan imefanikiwa kupindua matokeo na kupata ushindi wa 2-1, magoli ya Taifa Stars yalifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 49 goli ambalo la kusawazisha na dakika ya Ditram Nchimbi dakika ya 78 aliyeitwa dakika za jioni Taifa Stars baada ya kuifunga Yanga hart-trick akafunga goli la ushindi.

Matokeo yakamalizika kwa aggregate ya 2-2 lakini Tanzaia inafuzu fainali za CHAN baada ya kuwa imefunga magoli mengi ugenini, hii ni mara ya kwanza kwa Taifa Stars inafuzu kucheza fainali za CHAN toka 2009 ilivyofanya hivyo kwa kuitoa Sudan na kwenda Ivory Coast.

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments