Michezo

Neymar ataka refa aliyewachezesha na Napoli aadhibiwe

on

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil anayeichezea club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar ameomba refa wa mchezo aliyewachezesha kati ya PSG dhidi ya Napoli aadhibiwe kutokana na kitu alichomwambia.

Neymar katika mchezo huo uliyomalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, alipata nafasi ya kucheza kwa dakika zote 90, baada ya mchezo alionekana kukasirika kutokana na refa wa mchezo huo Bjorn Kuipers kudai alimtolea kauli ya kumvunjia heshima.

 

“Refa aliniambia kitu ambacho sina, ile ilikuwa ni kunivunjia heshima, sitaki kurudia nini alikisema kwangu, hata hivyo kwa mwingine angeweza kufanya kitu, hawezi kunivunjia heshima kama alivyonifanyia “>>>Neymar

Neymar alioneshwa kadi ya njano kipindi cha pili alipokuwa akijiandaa na mchezaji mwenzake Marco Verratti kupiga faulo lakini haijajulikana kama kauli hiyo, Neymar aliambiwa alipooneshwa kadi ya njano au wakati wa mchezo.

Licha ya PSG kuongoza kwa goli 1-0 lililofungwa na Juan Bernat dakika ya 45, Napoli walifanikiwa kusawazisha kwa penati dakika ya 62 kupitia kwa Lorenzo Insigne na kufanya mchezo umalizike 1-1, PSG wapo nafasi ya tatu kwa kuwa na point tano, Napoli nafasi ya pili kwa kuwa na point sita sawa na Liverpool anayeongoza Kundi hilo.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments