Michezo

Mambo magumu kwa Chelsea, Liverpool Bingwa wa UEFA Super Cup

on

Usiku wa August 14 ulikuwa ni usiku wa game ya Bingwa wa UEFA Europa League ambaye ni Chelsea dhidi ya Bingwa wa UEFA Champions League ambaye ni Liverpool, timu hizi zilikuwa zinakutana katika mchezo wa UEFA Super Cup katika uwanja wa Vodafone mjini Instanbul nchini Uturuki.

Ni game ambayo ilikuwa inazikutanisha timu zote za England na zinajuana vizuri kutokana na kucheza Ligi moja, kitu ambacho kilipeleka dakika 120 kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, magoli ya Liverpool yakifungwa na Sadio Mane dakika ya 48 na 95 huku ya Chelsea yakifungwa na Oliver Giroud dakika ya 36 na Jorginho kwa mkwaju wa penati dakika ya 101.

Baada ya dakika 120 kumalizika matokeo yakiwa 2-2, muamuzi wa kwanza wa kike Stephanie kuwahi kuchezesha mchezo wa wanaume unaondaliwa na UEFA aliamuru zipigwe penati kama sheria inavyotaka na Liverpool kuibuka na ushindi wa penati 5-4, pamoja na kumkosa golikipa wao namba moja kwa majeruhi Allison lakini golikipa wao mwingine Adrian aliibuka shujaa baada ya kufanikiwa kucheza penati ya Abraham na kuifanya Chelsea kuondoka vichwa chini.

Chelsea wakiwa chini ya kocha wao mpya na legend wa club hiyo Frank Lampard wanaendelea kuondoka uwanjani vichwa chini baada ya kupoteza mchezo wao wa pili mfululizo, baada ya kufungwa na Man United 4-0.

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments