Michezo

Spurs wameiua Man City, FC Porto hawajatoka salama Anfield

on

Game za mzunguuko wa kwanza wa robo fainali ya UEFA Champions League zimechezwa leo nchini England, usiku wa April 9 zimechezwa game mbili ambazo zilikuwa zinakutanisha timu tatu za England, Man City alikuwa ugenini kucheza dhidi ya Tottenham wakati Liverpool alikuwa nyumbani Anfield kuikaribisha FC Porto ya Ureno.

Mchezo wa Man City dhidi ya Tottenham ulimalizika kwa Tottenham kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Heung-Min Son dakika ya 78, wakati Liverpool nao wakiilaza FC Porto kwa magoli 2-0 yaliofungwa na Naby Keita dakika 5 na Firmino dakika ya 26 ya mchezo.

England ambao ndio wanakutanisha timu nyingi katika hatua hii ya robo fainali wakiingiza jumla ya timu nne (Tottenham, Liverpool, Man City na Man United) watalazimika kuziombea dua timu zao hili zifanye vizuri katika hatua hiyo japo moja italazimika kuishia hatua ya robo fainali 100%  (Man City na Tottenham) kwa kukutana wenyewe kwa wenyewe, mechi za April 10 ni Man United dhidi ya FC Barcelona na Ajax dhidi ya Juventus.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments