Michezo

Son Heung Min amlilia Andre Gomes kumchezea rafu ilimtoa na machela uwanjani

on

November 3 2019 ulichezwa mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Everton dhidi ya Tottenham Hotspurs, mchezo ambao ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1, goli la Everton likifungwa na Tosun dakika za nyongeza na Dele Alli kwa Tottenham dakika ya 63.

Mchezo huo kabla ya kumalizika lilitokea tukio la kuumiza uwanjani, kufuatia Son Heung Min kumchezea faulo Andre Gomes kiasi cha kuhofiwa kuwa mchezaji huyo amevunjika, huku wengine wakidai mfupa wa mguu umeama sehemu yake, bado inasubiriwa taarifa rasmi ya madaktari.

Son alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 79 lakini habari haikuwa kadi nyekundu, zaidi ya Son kuzidi kumwaga machozi kiasi cha kupelekea baadhi ya wachezaji wa Everton kumbembeleza, tukio hilo lilimfanya staa wa Tottenham raia wa Ivory Coast Serge Aurier kupiga magoti na kusali kwa huzuni.

Tukio hilo liliigusa hadi FC Barcelona ambao ukurasa wao wa twitter ulipost taarifa za kumtakia kila la kheri Gomes, uzito wa tukio hilo ulifanya Sky Sports kushindwa kuonesha marudio (Replay) kwani haikuwa rafu ya kawaida, kutokana na mchezaji huyo alivyoumizwa.

Kapombe kaanika sababu za kustaafu kuichezea Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments