Michezo

Zidane na Gareth Bale wadaiwa kupigana vijembe

on

Inaelezwa kuwa uhusiano kati ya kocha wa sasa wa Real Madrid Zinedine Zidane na mchezaji wake raia wa Wales Gareth Bale sio mazuri kiasi cha kuamini kuwa, Bale atalazimika kuondoka katika club hiyo kutokana na kutokuwa na nafasi na hata msimu ujao wa 2019/2020 anaweza hasipate nafasi ya kucheza chini ya Zidane na kuishia kuwa benchi tu.

Inaaminika kuwa leo katika mchezo wa mwisho wa kufungia msimu wa 2018/2019 kati ya Real Madrid dhidi ya Real Betis uliyomalizika kwa Real Madrid kupoteza kwa 2-0, ndio siku ambayo Gareth Bale ilikuwa game yake ya mwisho kuichezea Real Madrid kwani ataondoka, kutokana na kutokuwa chaguo la Zidane ambaye alithibitishia umma kuwa kunaweza kukawepo kwa tofauti kati yao.

Baada ya game kumalizika huku Zidane akidaiwa kutompa nafasi Gareth Bale kuaga mashabiki alieleza hivi mbele ya waandishi wa habari “Ni kweli sijampa nafasi (Bale) ya kuaga natakiwa kuangalia siku na siku kufanya maamuzi , kama kuna kitu sikipendi au sioni kama sahihi kukifanya nitafanya ninavyoona mimi ni sahihi, hata kama ningekuwa na nafasi nne za kufanya sub nisingemuingiza Gareth Bale kwa leo”>>>Zidane

Inadaiwa Bale akiwa katika benchi na wachezaji wenzake alitoa kauli kuwa “Bado nina mkataba wa miaka mitatu umebakia kama watataka mimi niondoke watatakiwa kunilipa euro milioni 17 kwa mwaka vinginevyo nitabaki haijalishi sipati nafasi ya kuchezi au vipi nitacheza golf”>>>Bale

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments