AyoTV

Juma Kaseja kakiri “Mpira mchezo wa Mbinu”

on

Club ya KMC leo ilicheza mchezo wake wa marudiano wa michuano ya Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya AS Kigali katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, KMC walikuwa wanacheza mchezo wa marudiano baada ya game ya kwanza mjini Kigali Rwanda kumalizika kwa sare ya 0-0.

KMC wameondolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa kwa magoli 2-1, hivyo safari ya ushiriki wao katika michuano hiyo inaishia hapo, baada ya kumalizika kwa mchezo nahodha wa KMC Juma Kaseja aliongea na waandishi wa habari kuhusiana na matokeo hayo.

“Kwanza naweza kusema namshukuru Mungu pili naweza kusema mpira ni mchezo wa mbinu sisi tumekuja na mbinu na wao wamekuja na mbinu, mbinu zao zimeenda ku-click ndani ya uwanja na wamepata matokeo kwa hiyo hamna haja ya kumlalamikia mtu, timu kama timu imefanya makosa mawili”>>> Kaseja

VIDEO: Niyonzima kaeleza kilichotokea kati yake na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments