Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mfanyabiashara Kylie Jenner pamoja na mzazi mwenzake Travis Scott penzi lao limeonekana kuwa na dosari baada ya kuelezwa kuwa wawili hao waliingia kwenye ugomvi mwezi uliopita.
Inaelezwa kuwa Kylie Jenner alidai kukuta ujumbe wenye ushahidi wa usaliti kwenye simu ya mpenzi wake Travis Scott na ndipo hapo ukaribu wao ulipoanza kufifia huku taarifa nyingine zikidai kuwa Kylie Jenner hana dalili za kumsamehe Travis na hivyo itakuwa ngumu kwa wawili hao kurudisha ukaribu waliokuwa nao kabla.
Inaripotiwa kuwa kwa sasa Kylie ampa mtoto wake Stormi kipaumbele zaidi pamoja na biashara zake za urembo (Kylie Cosmetics) na hataki mtu yeyote kuingilia vitu hivyo na ishu nzima ya kuweka sawa mahusiano yake na Travis Scott.
VIDEO: Siwezi kujichubua huo muda sina, Bongomovie wakongwe wanasumbua sana location’