Michezo

Ole Gunnar Solskjaer siku zake zinahesabika Old Trafford, Massimiliano Allegri ananyemelea ajira yake

on

Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabovu kwa club ya Man United kiasi cha kushika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu England, imeanza kuenea tetesi mitandaoni kuwa nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer katika club ya Man United inazidi kuwa finyu, awali zilitoka tetesi kuwa uongozi wa Man United umempa hadi kufikia mechi dhidi ya Norwich timu iwe imeimarika.

Leo mtandao wa dailymail umeripoti kuwa kocha wa zamani wa Massimiliano Allegri anadaiwa kuanza kuipigia chapuo nafasi ya ukocha wa Man United, kwa maana kwamba siku za Ole Gunnar Solskjaer ndani ya Old Trafford zinazidi kuhesabika, leo imeripotiwa kuwa Massimiliano Allegri amewaka nia kuwa akipewa kazi ya kuonoa Man United atamuongeza kwenye benchi lake la ufundi Patrice Evra.

Patrice Evra akiwa na kocha Massimiliano Allegri wakati wakiwa Juventus pamoja.

Evra amewahi kuichezea Man United misimu zaidi ya 7 toka pale alipojiunga na Man United 2006 akitokea Monaco, Massimiliano Allegri inadaiwa kuwa anafikiria hilo kutokana na Evra kuielewa zaidi Man United lakini pia anamfahamu amewahi kumfundisha Juventus na kutwaa nae mataji mawili, hivi karibuni Evra alitumia ukurasa wake wa twitter na kuandika kuwa uongozi wa Man United sasa ni wakati wao kuwaita wawasaidie.

Patrice Evra alicheza Man United kuanzia 2006 hadi 2014 na kutwaa mataji matano ya EPL na moja la UEFA Champions League, hivyo inadaiwa kurudi kwake Old Trafford kunaweza kuongeza kitu, Massimiliano Allegri ambaye hana timu toka alipojiuzulu kuifundisha Juventus, kwa sasa anahusishwa pia kuhitajika na Tottenham licha ya yeye binafsi kuonekana kuwa kama ameweka Man United kama ndio chaguo lake la kwanza.

VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA

Soma na hizi

Tupia Comments