Michezo

Ngorongoro Heroes wameamua, wamemalizana na Uganda

on

Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes leo imefanikiwa kuandika historia mpya Uganda kwa kupata ushindi wa 4-2 dhidi ya Uganda U-20, ushindi huo unaipeleka Ngorongoro Heroes hatua ya nusu fainali ya michuano ya CECAFA U-20.

Magoli ya Ngorongoro Heroes leo yalifungwa na Andrew Simchimba dakika ya 25 na 60 na Kelvin John dakika ya 88 na 90, wakati magoli pekee ya Uganda yakifungwa na Abdul Aziz dakika ya 46 na 74, mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Gulu nchini Uganda.

Ushindi huo umeipeleka Ngorongoro Heroes nusu fainali na kuendelea kuleta matumaini kwa Tanzania katika soka la vijana, Tanzania sasa imekuwa ikifanya vizuri katika soka ngazi ya vijana baada ya kuonekana mipango yake ya muda mrefu imezaa matunda.

VIDEO: Mwalubadu katua Bongo hii ilikuwa kabla ya kupata matoke Yanga na Zesco

Soma na hizi

Tupia Comments