Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetangaza rasmi kumfungia kujihusisha na soka Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda FUFA Moses Magogo, Magogo awali alitangaza kujiweka pembeni kwa miezi miwili li kupisha uchanguzi lakini FIFA imejiridhisha tayari.
Baada ya FIFA kujiridhisha kuwa Moses Magogo aliuza tiketi za fainali za Kombe la dunia 2014 kinyume na taratibu, imetangaza rasmi leo kumfungia kwa kipindi cha miezi miwili kujihusisha na masuala yoyote yale ya soka na faini ya Dola 10000 (Tsh milioni 23)
Kama utakuwa unakumbuka vizuri May 30 2017 mbunge wa jimbo la Makindye Magharibi Allan Ssewanyana alipeleka tuhuma FIFA kuwa Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda Moses Magogo aliuza kinyume na taratibu tiketi 177 za Kombe la Dunia 2014 zilizokuwa zimeelekezwa kuuzwa Uganda, Magogo anadaiwa kuuza tiketi hizo nje ya Uganda tofauti na FIFA walivyokuwa wamekusudia tiketi kila shirikisho kuwauzia wananchi taifa husika.
VIDEO: Uamuzi wa Simba SC kuhusu kudaiwa kugoma kwa Mkude, Erasto, Chama na Gadiel