Michezo

TOP 5: Hawa ndio mastaa wa soka walioingiza pesa nyingi msimu huu

on

Ligi mbalimbali barani Ulaya zinaelekea kumalizika kwa sasa na baadhi ya Ligi tumeshuhudia timu kadhaa zikianza kuonesha dalili za kuwa Mabingwa, lugha rahisi ni kuwa unaweza kusema msimu wa kikosi wa 2018/2019 unaelekea kumalizika na kwa Afrika tutaanza kushuhudia fainali za AFCON 2019.

Kuelekea kumalizika kwa msimu naomba nikusogezee TOP 5 ya mastaa wa soka walioingia pesa nyingi katika msimu wa 2018/2019, list hii imetolewa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na France Football ambao wanaaminika zaidi katika takwimu zao za soka.

  1. Lionel Messi wa FC Barcelona ndio anaongoza namba moja akiwa ameingiza kiasi cha euro milioni 130 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 336.
  2. Cristiano Ronaldo wa Juventus anaendelea kushindana tena na Lionel Messi ambaye wamekuwa wakichuana viwanjani kwa muda mrefu, Ronaldo ameingiza kiasi cha euro milioni 113 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 292.
  3. Staa wa Paris Saint Germain Neymar inawezekana mkataba wake wa ubalozo wa QNB unampa mkwanja mrefu kwani mwaka huu ameingiza kiasi cha euro milioni 91.5 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 236.
  4. Mshambuliaji tegemeo wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amefanikiwa kuingiza kiasi cha euro milioni 44 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 113.
  5. Gareth Bale wa Real Madrid ndio anahitimisha TOP 5 hii kwa kufanikisha kuingiza kiasi cha euro milioni 40.2 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 103.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments