Michezo

FC Barcelona imeanza vibaya LaLiga 2019/20, Super Sub Aduriz ndio kawamaliza

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania leo usiku wa August 16 2019 ilicheza mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Hispania LaLiga, Barcelona walicheza dhidi ya Athletic Bilbao lakini wachambuzi wa soka walikuwa wanaipa nafasi kubwa FC Barcelona kufanya vizuri katika mchezo huo uliomalizika kwa wao kupoteza 1-0.

Bilbao wakiwa nyumbani goli la dakika ya 89 lililofungwa na mkongwe Aritz Aduriz ndio limeiwezesha timu hiyo kubaki na point tatu, Barcelona ndio inakuwa timu ya kwanza kuanza na kipigo LaLiga na kuiacha Bilbao ikiongoza Ligi kwa muda ikiwa na point tatu.

Kikubwa kinachovutia katika mchezo huo ni kuwa mfungaji wa goli la ushindi Aritz Aduriz anayecheza nafasi ya ushambuliaji ametumia dakika moja tu kufanya maajabu, Aritz Aduriz mwenye umri wa miaka 38 katika mchezo huo dakika ya 88 na dakika ya 89 akafunga goli la ushindi la Bilbao na kuwaacha Barcelona wakianza safari ya Nou Camp wakiwa vichwa chini.

VIDEO: Mashabiki wanaoaminika kuwa wa Yanga waichanachana jezi ya Simba, Manara kafunguka

Soma na hizi

Tupia Comments