Habari za Mastaa

Taylor Swift akataa kujibu swali la Mwandishi

on

Mwimbaji wa Pop Taylor Swift amejikuta akikataa kujibu swali aliloulizwa kuhusiana na lini atapata mtoto akiwa mbioni kutimiza miaka 30 mwezi December swali hilo liliulizwa akiwa kwenye mahojiano na jarida la RTL Ujerumani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Complex nyota huyo wa Pop alikwepa swali na kutoa sababu akisema ‘Sidhani kama wanaume wanaulizwa swali kama hili wakifika miaka 30, hivyo siwezi kujibu swali hilo kwa sasa’ aliongozea na kusema kuwa ‘Nategemea kwenye miaka ya 30 tunajiskia sawa na jinsi tulivyo, kwa tinsi ninavyoikaribia ndio naona inafanyika”

Taylor Swift akiwa na mpenzi wake Joe Alwyn

Super staa huyo amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji Joe Alwyn’28 kwa miaka miwili sasa na amesema kuwa uzoefu wake kwenye miaka 20 ataenda nao mpaka kwenye miaka ya mbeleni.

VIDEO: MASIKINI ! SIKU 14 ZA SHAMIM NA MUMEWE GEREZANI, UPELELEZI KESI YAO HAUJAKAMILIKA

Soma na hizi

Tupia Comments